685- at-Twabaraaniy amepokea katika “al-Kabiyr” kupitia kwa Abu Maalik al-Ash´ariy aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ya ijumaa inafuta yale yaliyoko kati yake mpaka swalah ya ijumaa nyingine na ukiongezea na siku tatu. Kwa kuwa Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

مَن جَاء بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا

“Atayefanye tendo jema basi analipwa kumi mfano wake.”[1][2]

[1] 06:160

[2] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/431)
  • Imechapishwa: 20/01/2017