03. Hadiyth “Siku ya ijumaa Malaika hukaa kwenye milango ya misikiti… “


710- Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Siku ya ijumaa Malaika hukaa kwenye milango ya misikiti. Wanakuwa na madaftari yao ambayo wanawaandika watu. Wakati imamu anapotoka wanafunga madaftari yao.” Nikasema: “Ee Abu Umaamah! Si anamaanisha yule mwenye kutoka baada ya kuwa imamu amekwishatoka?” Nikasema: “Ndio, lakini hayuko katika wale wanaoandikwa katik madaftari.”[1]

Ameipokea Ahmad na at-Twabaraabiy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” na katika mlolongo wa wapokezi wake kuna Mubaarak bin Fadhwaalah.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/444)
  • Imechapishwa: 25/01/2018