586- Imepokelewa kutoka kwa Abu Ayyuub (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Milango ya mbingu hufunguliwa kwa ajili ya Rak´ah nne za kabla ya Dhuhr.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud na tamko ni lake na Ibn Maajah. Ameipokea pia at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” na “al-Mu´jam al-Awsatw:

“Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipotua kwangu nilimuona daima akidumu kuswali nne kabla ya Dhuhr. Akasema: “Pindi jua linapopondoka basi hufunguliwa milango ya mbingu. Hakuna mlango wowote unaofungwa mpaka kuswaliwe Dhuhr. Napenda katika saa hiyo kupandishwe kheri zangu.”[2]

[1] Nzuri kupitia zengine.

[2] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/380-381)
  • Imechapishwa: 09/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy