03. Hadiyth “Mfano wa ambaye amejifunza elimu… “

122- Abu Hurayrah amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mfano wa ambaye amejifunza elimu kisha asiizungumzie ni kama mfano wa ambaye anarundika hazina lakini hatoi kutoka katika hazina hiyo.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw”. Katika cheni ya wapokezi yuko Ibn Lahiy´ah[2].

[1] Nzuri na Swahiyh.

[2] Bi maana ni dhaifu. Lakini ni katika upokezi wa Ibn Wahb, kutoka kwa Ibn Lahiy´ah, kutoka kwa Darraaj Abus-Samh, kutoka kwa Abul-Haytham na ´Abdur-Rahmaan bin Hujayrah, kutoka kwa Abu Hurayrah. Cheni ya wapokezi ni nzuri kwa sababu masimulizi ya Ibn Lahiy´ah kutoka kwa Ibn Wahb ni Swahiyh. Pia masimulizi ya Darraaj ni Hadiyth nzuri kutoka kwa Ibn Hujayrah. Aidha Hadiyth hii ina njia nyenginezo na shawahidi zinazoipa nguvu. Nimeitaja katika ”as-Swahiyhah” (3479).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/160)
  • Imechapishwa: 05/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy