03. Hadiyth “Matendo yote ya mwanadamu ni yake, isipokuwa swawm… “

1081- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) amesema: “Matendo yote ya mwanadamu ni yake, isipokuwa swawm. Hiyo ni Yangu mimi na mimi Ndiye nitailipa. Swawm ni kinga. Itapokuwa ni siku ya funga ya mmoja wenu, basi asizungumze maneno machafu wala asipige kelele. Mtu akimtukana au akamgombeza, basi amwambie: “Mimi nimefunga. Mimi nimefunga.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na tamko ni lake, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy na Ibn Maajah.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/624-625)
  • Imechapishwa: 24/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy