03. Hadiyth “Haya ndio mmetumilizwa kwayo?”

140- Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Tulikuwa tumeketi nje ya mlango wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na tukibishana; mmoja anajengea hoja kwa Aayah moja na mwingine anajengea hoja kwa Aayah nyingine. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akajitokeza kwetu, uso wake umepiga wekundu kama mkomamanga, akasema: “Ee nyinyi! Haya ndio mmetumilizwa kwayo? Haya ndio mmeamrishwa? Msirejei baada yangu kuwa makafiri baadhi wakizipiga shingo za wengine.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy. Katika cheni ya wapokezi yuko Suwayd[2].

[1] Swahiyh kupitia zengine.

[2] Yaani Suwayd bin Ibraahiym Abu Haatim ambaye ana unyonge, kama ilivyo katika Hadiyth ilioko kabla yake. Lakini at-Twabaraaniy ameipokea tena kutoka kwa Anas na katika cheni ya wapokezi hiyo wapokezi wote ni waaminifu na imara, kama ilivyotajwa katika “Majma´-uz-Zawaaid” (01/157). Pia Ibn Maajah na Ahmad wameipokea kupitia kwa Ibn ´Amr kwa cheni ya wapokezi nzuri. Kwa hiyo Hadiyth ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/169)
  • Imechapishwa: 07/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy