03. Hadiyth “Hakika wale waliokuwa kabla yenu katika watu wa Kitabu walifarikiana… “

51- Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituhutubia akasema: “Hakika wale waliokuwa kabla yenu katika watu wa Kitabu walifarikiana makundi sabini na mbili, na Ummah huu utafarikiana makundi sabini na tatu. Makundi sabini na mbili yataingia Motoni na moja litaingia Peponi. Nalo ni Mkusanyiko[1].”[2]

Ameipokea Ahmad na Abu Daawuud ambaye amezidisha:

“Katika Ummah wangu watajitokeza watu wanaopatwa na matamanio kama ambavo maradhi ya kichaa yanavompata mwenye nayo; hayatoacha kiungo wala mshipa wowote isipokuwa utaingia ndani yake.”[3]

[1] Bi maana Maswahabah, kama ilivyokuja katika mapokezi mengine. Katika upokezi mwingine imekuja:

”Ni lile linalofuata yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”

Ameipokea at-Tirmidhiy na wengineo. Nimeitoa katika mjeledi wa kwanza. Mtu analazimika kutambua kuwa kushikamana na njia yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio dhamana pekee kwa muislamu asipotee kwenda kuliani na kushotoni. Ni jambo ambalo wameghafilika kwalo vyama vingi ya Kiislamu, sembuse mapote potevu.

[2] Nzuri na Swahiyh.

[3] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/129)
  • Imechapishwa: 27/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy