739- Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

“Nilikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika safari miongoni mwa safari ambapo nikawa karibu naye na huku tunasafiri.  Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nijuze juu ya kitendo kitachoniingiza Peponi na kitanitenga mbali na Moto?” Akasema: “Hakika umeuliza juu ya jambo kubwa, lakini ni jepesi kwa yule aliyewepesishiwa na Allaah; mwabudu Allaah na wala usimshirikishe Yeye na chochote, simamisha swalah, toa zakaah, funga Ramadhaan na uhiji Nyumba.”[1]

Ameipokea Ahmad, at-Tirmidhiy ambaye ameihihisha, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah.

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/456)
  • Imechapishwa: 12/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy