03. Hadiyth “Allaah ampambe mtu ambaye amesikia maneno yangu… “

91- Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitutolea Khutbah kwenye msikiti wa Khayf huko Minaa ambapo akasema:

“Allaah ampambe mtu ambaye amesikia maneno yangu ambapo akayahifadhi, akayaelewa kisha akamfikishia yule ambaye bado hajayasikia. Huenda ambaye amebeba uelewa yeye mwenyewe sio mwelewa. Huenda ambaye amebeba uelewa akamfikishia ambaye ana uelewa zaidi kuliko yeye.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw”.

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/147-148)
  • Imechapishwa: 01/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy