03. Faradhi ya kwanza kwa watoto


Kitu cha kwanza Allaah kukifaradhisha kwa waja ni kukufuru Twaaghuut na kumuamini Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaaghuut.”[1]

Twaaghuut ni:

1- Kila chenye kuabudiwa badala ya Allaah.

2- Shaytwaan.

3- Kuhani.

4- Mnajimu.

5- Anayehukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah.

6- Kila mwenye kufuatwa na kutiiwa katika kitu kisichokuwa haki. ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

Twaaghuut ni kila chenye kuabudiwa, kufuatwa na kutiiwa ambacho mja amepindukia kwacho mipaka.”[2]

[1] 16:36

[2] I´laam-ul-Muwaqqi´iyn (1/5).

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liym-us-Swibyaan at-Tawhiyd, uk. 15-16