Allaah (Ta´ala) amesema:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.” (20:05)

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“… kisha akalingana juu ya ´Arshi.” (07:54)

[Matamshi kama haya yamekuja] sehemu sita katika Qur-aan. Nazo ni:

1- al-A´raaf Aayah ya 54

2- Yuunus Aayah ya 03

3- ar-Ra´d Aayah ya 02

4- al-Furqaan Aayah ya 59

5- al-Sajdah Aayah ya 04

6- al-Hadiyd Aayah ya 04

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ

“Naye ni Mshindi Mwenye kudhibiti [aliye] juu ya waja Wake.” (06:18)

يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ

“Wanamkhofu Mola wao Aliye juu yao na wanafanya yale wanayoamrishwa. “ (16:50)

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake pekee linapanda neno zuri na kitendo chema hukipa hadhi.” (35:10)

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pindi Allaah alipoumba viumbe aliandika katika Kitabu Chake kilichoko juu ya ´Arshi: “Hakika huruma Wangu unashinda ghadhabu Zangu”.” al-Bukhaariy (3022) na Muslim (2721)

Mu´aawiyah al-Hakamiy as-Sulamiy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Mimi nilikuwa na mjakazi ambaye alikuwa akinichungia mbuzi zangu upande wa Uhud na Jawaaniyah. Siku moja akaja hali ya kuwa mbwa mitu amechukua mbuzi mmoja. Mimi ni mwanaadamu nakasirika na kuhuzunika kama wanavyokasirika wengine. Nikawa nimemtia adhabu kweli kweli. Nikaja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na jambo hilo likawa kubwa. Nikamwambia: “Ee Mtume wa Allaah! Si nimwache huru?” Akasema: “Niletee naye.” Nikaja naye mpaka kwa Mtume. Mtume akamwambia: “Allaah yuko wapi?” Mjakazi akajibu: “Mbinguni.” Akamuuliza tena: “Mimi ni nani?” Akajibu: “Wewe ni Mtume wa Allaah.” Mtume akasema: “Mwache huru, kwani hakika ni muumini”.” Muslim (537)

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qawl al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd
  • Imechapishwa: 05/08/2020