03. al-Albaaniy ni mwanachuoni wa kipekee


Amemtuhumu al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kwamba anamfuata kichwa mchunga Sayyid Qutwub katika utangulizi wake wa “Mukhtaswar-ul-´Uluww” ambapo amemnukuu:

“Sisi hii leo tunaishi katika kipindi cha kikafiri kama kile kipindi kilichokuwepo mwanzoni mwa Uislamu au chenye giza zaidi. Mambo yote yaliyotuzunguka ni ya kipindi cha kikafiri; fikira za watu, ´Aqiydah zao, desturi zao, marejeo ya tamaduni zao, sanaa zao, adabu zao, Shari´ah zao mpaka mengi katika yale tunayozingatia ni tamaduni na marejeo ya Kiislamu.”[1]

Mosi ni batili na uongo kusema kwamba al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) anamfuata Sayyiq Qutwub kichwa mchunga. Mwandishi amechukua nukuu hii ambapo akamhukumu al-Albaaniy kwamba anamfuata Sayyid Qutwub kichwa mchunga. Sijui lengo ni lipi la kumchafua mtu ambaye vitabu vyake vilivyoitumikia Sunnah ya kinabii vimejaa maduka ya vitabu. Amebainisha Hadiyth Swahiyh na dhaifu na ametumia zaidi ya miaka khamsini akifanya kazi hiyo. Ametunga mijaladi mingi katika maudhui hayo. Hivi kweli inawezekana kitu kama hicho akafanyiwa mtu ambaye ameitumikia Sunnah kwa njia ya kipekee na ambayo tunaamini kwamba ni katika wanachuoni bora ambayo wamepambana katika kuieneza dini ya haki? Haya ndio tunayotambua na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Si yeye wala mwanachuoni mwingine yeyote, vovyote atavyokuwa na elimu, hatuamini kuwa amekingwa na kukosea. Vovyote mtu atavyokuwa na elimu mapungufu ya kiuanaadamu hayakosi kwa mtu.

[1] Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 61

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 21/10/2018