03. Adabu ya tatu: kuukaribisha moyo na elimu


Ni juu ya mwanafunzi ahakikishe hamu yake kubwa iwe Aakhirah na vile vilivyo huko kwa Allaah. Anatakiwa awe amefungamana na malengo ya hali ya juu. Hakika ya elimu inamshughulisha mtu na vipumbazo vya kimaisha. Hakika maisha ni masiku machache tu…

Mwanafunzi anatakiwa kukata vitu vyote vya kushughulisha. Hakika fikira zinapotawanyika basi zinakuwa na upungufu wa kudiri uhakika wa mambo. Salaf walikuwa wakiipa kipaumbele elimu juu ya kila kitu. Imesimuliwa kutoka kwa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) kwamba hakuoa isipokuwa baada ya miaka arubaini. ash-Shaafi´iy amesema:

“Hakuna yeyote anayetafuta elimu hii kwa kutaka ufalme na starehe ya nafsi kisha akafaulu. Lakini mwenye kuitafuta kwa moyo mdhalilifu, maisha mafumu na kuwatumikia waalimu ndio hufaulu.”

Ibn Wahb amepokea kutoka kwa Maalik bin Anas (Rahimahu Allaah) ya kwamba amesema:

“Hakuna yeyote anayeifikia elimu hii kile kiwango anachotaka isipokuwa mpaka ufakiri umpige na aipe kipaumbele juu ya kila kitu.”

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Sa´iyd Raslaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadab Twaalib-ul-´Ilm, uk. 45-62
  • Imechapishwa: 23/04/2017