03. Mume anatakiwa kumfanyia upole mkewe

1- Kumfanyia upole mke wakati wa kukutana naye kinyumba

Imependekezwa wakati atapomwingilia mke wake basi amfanyie upole kama vile kuanza kumpa kitu katika kinywaji na kitu mfano wake. Dalili ya hilo ni Hadiyth ya Asmaa´ bint Yaziyd bin as-Sakan ambaye amesimulia:

“Mimi nilimpamba ´Aaishah kwa ajili ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Halafu nikamwita aje kumwangalia na kumfunua ambapo akawa amekuja na kukaa pembezoni mwake. Akaleta kikombe kikubwa cha maziwa ambapo akaanza kunywa yeye kisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwelekezea nacho ambapo akaona haya na kuinamisha kichwa kwa kuona haya.” Asmaa´ anasema: “Nikamgombeza na kumwambia: “Kipokee kutoka kwenye mikono yha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)” ambapo akafanya hivo na kunywa kidogo. Kisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mengine wape marafiki zako.” Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Yachukue wewe uyanywe kisha nipokeze kwa mikono yako”. Akayachukua na kuyanywa kisha akanipokeza. Nikakaa chini kisha nikayaweka kwenye magoti yangu halafu nikaanza kukifuatisha kwa mdomo wangu hali ya kukizungusha ili ninywe pale alipokunywa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akasema juu ya wale wanawake wengine waliokuwa na mimi: “Wape wenzako.” Wakasema: “Hatuyataki.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Msichanganye njaa na uongo.”[1]

[1] Ahmad (06/438) kwa kirefu na kwa kifupi kwa sanadi mbili kila moja inaipa nguvu nyingine. al-Mundhiriy ameashiria kuwa kwake na nguvu (04/29) na al-Humaydiy vilevile amefanya hivo katika “al-Musnad” yake (02/61). Vilevile ina shawahidi katika “at-Twabaraaniy” katika “as-Swaghiyr” na “al-Kabiyr” “Taariyh Aswbahaan” ya Abiysh-Shaykh 282-283 na kitabu “as-Swamt” (02/26) ya Ibn –ud-Dunyaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 91-92
  • Imechapishwa: 23/02/2018