02. Waumini wanamuamini Allaah kwa miili yao, nyoyo zao na ndimi zao

Imani ni maneno na vitendo. Haya yanathibitishwa na Qur-aan na Sunnah. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu kupanda kwa imani:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا ۚ لَّهُمْ دَرَجَاتٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَمَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ

“Hakika waumini ni wale ambao anapotajwa Allaah nyoyo zao zinajaa khofu na wanaposomewa Aayah Zake huwazidishia imani na kwa Mola wao wanategemea; ambao wanasimamisha swalah na katika yale Tuliyowaruzuku hutoa; – hao ndio waumini wa kweli. Wana daraja za juu kwa Mola wao na msamaha na riziki tukufu [zinawasubiri].” 08:02-04

Katika Aayah hizi Allaah amefafanua waumini walio na imani kamilifu na wenye imani ya kweli:

الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ

“… ambao anapotajwa Allaah nyoyo zao zinajaa khofu… “

Haya ni matendo ya moyo. Pindi muumini anapomfikiria Allaah wakati wa dhambi anashikwa na woga na anaiacha. Au anamkumbuka Allaah na hilo linamfanya kuwa na woga:

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

“Hakika wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni wanachuoni.” 35:28

Wanamcha Allaah kikamilifu. Kumwogopa na kumcha Allaah ni sifa alio nayo daima. Huyu ndiye muumini, haya ni matendo ya moyo.

وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا

“… na wanaposomewa Aayah Zake huwazidishia imani… “

Hii ni dalili ya kuzidi kwa imani. Aayah hii, seuze Hadiyth zengine, inamtosha kwa mtu aliye na tabia na anakiheshimu Kitabu cha Allaah.

وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ

“… na kwa Mola wao wanategemea…”

Haya ni matendo ya moyo.

الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ

“… ambao wanasimamisha swalah na katika yale Tuliyowaruzuku hutoa… “

Haya ni matendo ya viungo vya mwili.

أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا

“… hao ndio waumini wa kweli.”

Imani yao ni ya kweli. Allaah amewashuhudilia.

دَرَجَاتٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَمَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ

“Wana daraja za juu kwa Mola wao na msamaha na riziki tukufu [zinawasubiri].”

Haya ndio malipo yao. Wamemuamini Allaah kwa miili yao, nyoyo zao na ndimi zao.

Kwa hivyo imani ni maneno, matendo na kuamini. Inazidi kwa matendo mema na inapungua kwa maasi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 07-08
  • Imechapishwa: 09/10/2016