Katika jumla ya wema waliotangulia ambao walikuwa wakifuata ´Aqiydah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah wake na Taabi´uun, walikuwa ni maimamu wanne: Imaam Abu Haniyfah, Imaam Maalik, Imaam ash-Shaafi´iy na Imaam Ahmad. Walisimama wakiitetea ´Aqiydah hii, wakaiandika na kuwafunza nayo wanafunzi.

Wafuasi wa maimamu hawa walikuwa wakiitilia umuhimu ´Aqiydah hii. Walikuwa wakiidurusu, wakiwahifadhisha nayo wanafunzi na watoto wao na wakatunga vitabu vingi kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah; yale aliyosimama kwayo mteule (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake (Radhiya Allaahu ´anhum) na Taabi´uun. Wakaraddi I´tiqaad batili na zilizopinda na wakabainisha ubatilifu wake. Vivyo hivyo ndivo walivofanya maimamu wa Ahl-ul-Hadiyth akiwemo Ishaaq bin Raahuyah, al-Bukhaariy, Muslim, Imaam Ibn Khuzaymah na Imaam Ibn Qutaybah.  Vilevile maimamu wa tafsiri za Qur-aan, kama vile Imaam at-Twabariy, Imaam Ibn Kathiyr na Imaam al-Baghawiy. Wameandika vitabu vinavyoitwa “as-Sunnah”, kama mfano wa “as-Sunnah” ya Ibn Abiy ´Aaswim, “as-Sunnah” ya ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal, “as-Sunnah” ya al-Khallaal na “ash-Shariy´ah” ya al-Aajurriy.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 22-26
  • Imechapishwa: 05/08/2018