02- Anatakiwa awe kati ya kuogopa na kutaraji. Kwa msemo mwingine ni kwamba aogope adhabu ya Allaah juu ya madhambi yake na wakati huohuo atarajie huruma ya Mola Wake. Hayo ni kutokana na Hadiyh ya Anas:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia kwa kijana ambaye alikuwa katika hali ya kukata roho ambapo akamuuliza: “Unaendeleaje?” Akajibu: “Ee Mtume wa Allaah! Ninaapa kwa Allaah kwamba nataraji kwa Allaah na nakhofia juu ya madambi yangu.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Hayakusanyiki kwenye moyo wa muumini katika hali kama hii isipokuwa Allaah atampa kile alichotarajia na atamuepusha na kile anachogopa.”

Ameipokea at-Tirmidhiy na cheni ya wapokezi wake ni nzuri, Ibn Maajah, ´Abdullaah bin Ahmad katika “Zawaaid az-Zuhd”, uk. 24-25, Ibn Abiyd-Dunyaa katika ilivyo katika “at-Targhiyb” (04/141). Tazama “al-Mishkaah” (1612).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 03
  • Imechapishwa: 25/12/2018