02. Sherehe ya nusu ya Sha´baan haina msingi katika dini


Miongoni mwa Bid´ah zilizozuliwa na watu ni Bid´ah ya kusherehekea usiku wa nusu ya Sha´baan na kufanya usiku wake ni maalum kwa ajili ya kufunga. Hayo hayana dalili inayofaa kutegemewa. Kumepokelewa juu yake Hadiyth ambazo ni dhaifu haijuzu kuzitegemea. Kuhusu yale yaliyopokelewa juu ya ubora wake yote yamezuliwa. Hayo yamezinduliwa na wanazuoni wengi. Nitataja baadhi ya maneno yao – Allaah akitaka.

Vilevile kumepokelewa juu yake baadhi ya Aathaar kutoka kwa baadhi ya Salaf kutoka Shaam na kwenginepo. Yale wanayoonelea wanazuoni wengi ni kwamba kuisherehekea ni Bid´ah na kwamba Hadiyth zilizopokelewa juu ya fadhilah zake zote ni dhaifu na nyenginezo zimetungwa. Hayo yamezinduliwa na Haafidhw Ibn Rajab katika kitabu chake “Latwaaif-ul-Maa´arif” na venginevyo.

Hadiyth dhaifu zinatendewa kazi katika ´ibaadah ambazo msingi wake umethibiti kwa dalili sahihi. Kuhusu kusherehekea usiku wa nusu ya Sha´baan ni jambo halina msingi sahihi ili mtu aweze kujiliwaza kwa Hadiyth ambazo ni dhaifu. Kanuni hii tukufu imetajwa na Imaam Abul-´Abbaas Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr minal-Bid´ah, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 16/01/2022