Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Sharti ya pili ni kuwa na akili na kinyume chake ni wendawazimu. Mwendawazimu kalamu yake imesimamishwa mpaka anapopata akili. Dalili ni Hadiyth:

“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu aina tatu; aliyelala mpaka anapoamka, mtoto mpaka anapobaleghe na mwendawazimu mpaka anapopata akili.”[1]

MAELEZO

Mtu anatakiwa kuwa na akili ambayo kwayo anapambanua kati ya yale yenye kumnufaisha na yenye kumdhuru na kati ya kheri na ya shari. Ama mtu akiwa mwendawazimu au ana ugonjwa wa akili ambapo hawezi kupambanua mambo, basi swalah yake si sahihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallamm) amesema:

“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu aina tatu; aliyelala mpaka anapoamka, mtoto mpaka anapobaleghe na mwendawazimu mpaka anapopata akili.”

[1] Abu Daawuud (4405) na Ahmad (1362). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2/5).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 63
  • Imechapishwa: 24/06/2018