02. Ni lazima kuamini wasifu wa Mtume kumsifia Allaah


Pia zile sifa nyenginezo zote ambazo mteule (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemsifu kwazo kama mfano wa:

1 – Ameipanda Pepo ya Firdaws na Twuubaa kwa mkono Wake.

2 – Ameiandika Tawraat kwa mkono Wake.

3 – Ataweka unyayo Wake juu ya Moto ambapo utasema: ”Tosha, tosha.”

4 – Anavyo vidole.

5 – Anacheka.

6 – Anastaajabu.

7 – Anashuka kila usiku, usiku wa ijumaa, usiku wa nusu Sha´baan na usiku wa Qadr.

8 – Ana ghera.

9 – Anafurahi kwa kutubu kwa mja Wake.

10 – Pazia Yake ni nuru.

11 – Shuka ya juu ya kiburi ndio imemzuia.

12 – Allaah sio chongo.

13 – Allaah anakipa mgongo kile anachokichukia na hakitazami.

14 – Mikono Yake yote ni ya kuume.

15 – Aadam alichagua kukamata Kwake kwa mkono wa kuume.

16 – Anakamata.

17 – Kila siku hutazama katika Ubao uliohifadhiwa.

18 – Ana vigawanyo vitatu kwa kiganja Chake cha mkono.

19 – Pindi Allaah (´Azza wa Jall) alipomuumba Aadam alipararaza uti wa mgongo Wake kwa mkono Wake wa kuume ambapo akakamata mikamato miwili, mkatamano mmoja wa upande wa kuume na mkatamano mwingine upande wa kushoto. Akasema kuwaambia wale waliokuweko katika mkono Wake wa kuume: ”Ingieni Peponi na wala sijali!” na akawaambia wale waliokuweko katika mkono Wake wa kushoto: ”Ingieni Motoni na wala sijali!” Kisha akawarudisha kwenye uti wa mgongo wa Aadam (´alayhis-Salaam).

20 – Imekuja katika Hadiyth ya kukamata ifuatavyo:

”Kisha ataushika Moto kwa mshiko ambapo awatoe nje wale watu waliochomwa. Watatupwa ndani ya mto karibu na maingilio ya Pepo kwa jina ´Maji ya uhai`.”[1]

21 – Imekuja katika Hadiyth ya kiganja Chake cha mkono wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipopandishwa safari ya mbinguni:

”Akaweka kiganja Chake cha mkono kati ya mabega yangu mpaka nikahisi ubaridi wa ncha ya vidole Vyake kati ya matiti yangu.”[2]

22 – Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Nimemuona Mola wangu katika sura nzuri kabisa.”[3]

23 – Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Amemuumba Aadam kwa sura Yake.”[4]

24 – Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Usiukebehi uso. Kwani hakika Allaah alimuumba Aadam kwa sura ya Mwingi wa rehema (´Azza wa Jall).”[5]

[1] al-Bukhaariy (7439) na Muslim (183).

[2] at-Tirmidhiy (3235) ambaye amesema:

”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.  Nilimuuliza Muhammad bin Ismaa´iyl juu yake akasema: ”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

[3] at-Tirmidhiy (3235) ambaye amesema:

”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.  Nilimuuliza Muhammad bin Ismaa´iyl juu yake akasema: ”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

[4] al-Bukhaariy (2560) na Muslim (2612).

[5] ad-Daaraqutwniy katika “Kitaab-us-Swifaat” (50).

  • Mhusika: Imaam Abul-Qaasim Sa´d bin ´Aliy bin Muhammad az-Zinjaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ajwibah fiy Usuul-id-Diyn, uk. 65-73
  • Imechapishwa: 14/06/2021