02. Namna hii ndivyo yanatakiwa kuanzwa maisha ya ndoa

Itambulike kuwa kuna adabu nyingi za ndoa. Yaliyotushughulisha katika uandishi huu wa haraka ni yale yaliyothibiti katika Sunnah ya Mtume Muammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) iliyotakasika ambayo hakuna nafasi yoyote ya kuyapinga kwa njia ya milolongo ya wapokezi wake au mtu akajaribu kuyatilia shaka kwa njia ya muundo wake. Lengo ni yule atakayesimama nayo awe juu ya elimu kutokamana na dini yake na uaminifu wa jambo lake. Mimi natarajia na kumuombea kwa Allaah amkhitimishe kwa furaha na iwe ni sababu ya kuyaanza maisha yake ya ndoa kwa kufuata Sunnah na amjaalie kuwa miongoni mwa wale waja wake ambao amewasifu kwa kusema:

رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا

“Ee Mola wetu! Tutunukie katika wake zetu na kizazi chetu viburudisho vya macho yetu na tujaalie kuwa ni waongozi kwa wachaji.”[1]

Mwisho mwema ni kwa wale wanaomcha Allaah, kama alivyosema Mola wa walimwengu:

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ

“Hakika wachaji wamo katika vivuli na chemchem na matunda katika yale wanayoyatamani.”[2]

 Adabu zenyewe ni hizi zifuatazo:

[1] 25:74

[2] 77: 41-44

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 89-90
  • Imechapishwa: 22/02/2018