Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimhu Allaah) amesema:

na kubainisha kinyume chake ambacho ni kumshirikisha Allaah.

MAELEZO

Kinyume cha Tawhiyd ni kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jall). Tawhiyd ni kumpwekesha Allaah katika ´ibaadah na shirki ni kufanya kitu miongoni mwa aina za ´ibaadah kumfanyia asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall). Mfano wa hayo ni kuchinja, kuweka nadhiri, kuomba du´aa, uokozi na aina nyinginezo za ´ibaadah. Hii ndio shirki. Makusudio ya shirki ni katika ´ibaadah. Ama kuhusu shirki katika Rubuubiyyah ni kitu kisichokuwepo mara nyingi. Watu wote ni wenye kuikubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Hili hawana namna ya kulikwepa. Mwenye kuipinga anajidhihirisha hivyo pamoja na kuwa wakati huohuo anaikubali ndani ya moyo wake. Kwa sababu kuikubali ni kitu kisichokuwa na budi. Kila mtu anajua kuwa viumbe hivi na ulimwengu huu ni lazima uwe na Muumbaji na ulimwengu huu unaoenda ni lazima uwe na mwendeshaji. Ulimwengu huu hauko bure tu hivihivi kwa dhati yake:

أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ

“Au wameumbwa pasipo na kitu chochote au wao [wenyewe] ndio waumbaji? Au wameumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini. (53:35-36)

Kukubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ni kitu cha kilazima na tena cha kimaumbile. Hata hivyo ni kitu kisichotosheleza. Kule washirikina kuikubali hakukuwatosheleza kitu kama ilivyotajwa katika Qur-aan. Qur-aan imetaja jambo hili waziwazi:

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ

“Na ukiwauliza: “Ni nani kawaumba?”

Wanajibu nini?

Wanajibu kwa kusema:

اللَّـهُ

“Allaah.” (43:87)

Bi maana Allaah Ndiye ambaye ametuumba. Hii ndio Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Kinachotakikana ni Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Hapa ndipo kulitokea tofauti na magomvi baina ya Mitume na nyumati zao, wenye kulingania katika dini ya Allaah na watu. Mizozo, mapambano, kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allaah na mengineyo yanapatikana katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah.

  • Mhusika: maam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 18/05/2021