Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

01 – Kushirikisha katika ´ibaadah ya Allaah (Ta´ala). Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa, lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”[1]

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ

“Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah atamharamishia Pepo na makazi yake yatakuwa ni Motoni – na madhalimu hawatopata mwenye kunusuru yeyote.”[2]

Katika hayo kunaingia pia kumchinjia asiyekuwa Allaah, kama ambaye anamchinjia jini au kaburi.

MAELEZO

Hiki ndio kichenguzi cha kwanza cha Uislamu. Nacho ni kushirikisha katika ´ibaadah ya Allaah (Ta´ala).

Utambulisho wa shirki:

Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab amesema alipokuwa anatambulisha shirki: kumtekelezea aina ya ´ibaadah asiyekuwa Allaah, kumuomba mwingine panoja na Allaah au ukamkusudia kwa mambo mengine katika aina za ´ibaadah ambazo Allaah ameamrisha[3].

Dalili ya kwanza kuhusu hukumu ya mshirikina duniani ni maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa, lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”

Kwa hiyo dhambi yake haisamehewi. Makusudio hapa ya neno “shirki” kunamaanishwa shirki kubwa. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) amefanya kuwa ni maalum na kulifungamanisha. Amefanya shirki kuwa ni maalum ya kwamba haisamehewi na akafungamanisha yaliyo chini ya shirki na utashi Wake.

Dalili ya pili ni kuhusu hukumu yake Aakhirah. Hukumu yake Aakhirah ni kwamba Pepo kwa mshirikina ni haramu kwake na atadumishwa Motoni milele. Amesema (Ta´ala):

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ

“Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah atamharamishia Pepo na makazi yake yatakuwa ni Motoni – na madhalimu hawatopata mwenye kunusuru yeyote.”

[1] 04:47

[2] 05:72

[3] Mu´alafaat-ush-Shaykh qism-il-´Aqiydah, uk. 281.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tabswiyr-ul-Anaam bisharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 09/04/2023