Miongoni mwa madhara yake mengine ni kwamba inazuia riziki. Katika “al-Musnad” kumepokelewa:

“Mja anapokonywa riziki kwa kutokana na dhambi aliyoifanya.”[1]

Kama ambavyo kumcha Allaah kunaleta riziki, kuacha kumcha Allaah kunaleta ufukara. Hakuna kitu kinachosababisha kuletwa kwa riziki ya Allaah kama kuacha maasi.

[1] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Ibn Maajah”, uk. 12.

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 65
  • Imechapishwa: 28/12/2017