Jina la “Allaah” ni ufahamisho wa dhati tukufu. Hakuna mwengine mwenye kuitwa hivo zaidi Yake (Subhaanahu wa Ta´ala). Hata wajeuri na makafiri hawajiiti hivo. Hakuna mwenye kujiita “Allaah”. Fir´awn alisema:

فأَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ

“Mimi ni mola wenu mkuu.”[1]

Hakusema kuwa yeye ni Allaah. Pamoja na ukafiri wake hakuwa na ujasiri wa kujiita jina hilo. Ni jina maalum kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Jina “Allaah” maana yake ni “Yule mwenye uungu”, bi maana mwenye kuabudiwa. Viumbe wote wanawajibika kumwabudu Yeye, kama alivosema Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa)[2].

[1] 79:24

[2] Jaami´-ul-Bayaan (1/45).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 20
  • Imechapishwa: 06/08/2019