Katika lugha ya Taurati na Injili kila mmoja ambaye ni mwema na mchamungu anaitwa “Mwana wa mungu”. Katika Matayo ya Injili imekuja:

“9Kila mwenye kufanya amani,

wanatakiwa kuitwa wana wa Mungu.

10Kila mwenye kuteswa kwa kutenda haki,

ufalme wa mbinguni ni wake.”[1]

Katika mlango huo huo mna:

“44Lakini mimi nawaambia: wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowaudhi; 45ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni.”[2]

“48Inawapasa muwe wakamilifu, kama jinsi Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.”[3]

“1Angalieni msifanye wema wenu machoni mwa watu, ili wakutazameni. Mkifanya hivyo hamtopata thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.”[4]

[1] Matayo 05:09-10

[2] Matayo 05:44-45

[3] Matayo 05:48

[4] Matayo 06:01

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy al-Maghribiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Baraahiyn al-Injiylyyah ´alaa anna ´Iysaa daakhil fiyl-´Ubuudiyyah wa la hadhdhwa lahu fiyl-Uluuhiyyah, uk. 12
  • Imechapishwa: 16/10/2016