Maana yake ni kuwa hakuna mwenye kufuatwa kwa haki isipokuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusu siyekuwa Mtume wa Allaah, endapo mtu huyo atafuatwa katika lisilokuwa na dalili, basi atakuwa amefuatwa kwa batili. Allaah (Ta´ala) amesema:

اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ

“Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu na wala msifuate badala Yake wasaidizi wengine. Ni machache mnayoyakumbuka.” (07:03)

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Basi Naapa kwa Mola wako ya kwamba hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kwa kujisalimisha kabisa.” (04:65)

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا

“Na haiwi kwa muumini mwanamme wala kwa muumini mwanamke, Anapohukumu Allaah na Mtume Wake amri yoyote ile, iwe wana khiari katika amri yao. Na anayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi kwa yakini amepotea upotofu bayana.” (33:36)

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qawl al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd
  • Imechapishwa: 05/08/2020