2- at-Twahaawiy (kfrk. 321) tabaka 11

adh-Dhahabiy ameandika wasifu wake katika ”Tadhkirat-ul-Huffaadhw” na akasema:

”Imaam, ´Allaamah, Haafidhw na mtunzi wa vitabu vizuri Abu Ja´far Ahmad bin Muhammad bin Salaamah bin Salamah al-Azdiy al-Hijriy al-Miswriy at-Twahaawiy al-Hanafiy. Twahaa ni mji huko Misri.

Alisafiri kwenda Shaam mwaka wa 268 kwa ajili ya kusoma chini ya qaadhi Abu Khaazim na wengineo.

Ibn Yuunus amesema:

”Alizaliwa mwaka wa 237 na alikuwa mwaminifu, imara, Faqiyh na mwenye busara. Hakuacha baada yake mtu mfano wake.”

adh-Dhahabiy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Abu Ja´far alitunga tofauti za wanachuoni, sharti, hukumu za Qur-aan na kitabu  ”Ma´aaniy al-Aathaar”. Alikuwa ni mtoto wa dadake al-Muzaniy.

Ibn Yuunus amesema:

”Abu Ja´far alifariki mwanzoni mwa Dhul-Qa´dah mwaka wa 321, akiwa na zaidi ya miaka 80.”

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tadhkiyr-un-Naabihiyn, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 04/02/2019