02. Kutofautiana kwa watu katika kuihakikisha furaha

Ni jambo linalojulikana na kila mtu anatamani kupatikane furaha nyumbani kwake. Lakini hata hivyo njia za watu zinatofautiana katika kuhakikisha furaha hii.

Kuna miongoni mwa watu wanaodhani furaha inapatikana katika kukusanya pesa. Watu kama hawa utawaona hamu yao kubwa ni kukithirisha pesa, kutafuta kuikuza mali yake na akaitelekeza familia yake. Muda mwingi hawamuoni na hawaulizii. Anapoulizwa ni kwa nini haiangalii familia yake, anauliza kwa kushangaa ni vipi mimi siitazami familia yangu ilihali nahangaika kwa ajili ya kuwaletea familia pesa. Kwa hivyo hawahakikishii si wao wala yeye mwenyewe furaha.

Kuna miongoni mwa watu wanaodhani furaha ya familia inapatikana peke yake katika kuzaa watoto wengi. Hivyo anafanya bidii kuzaa watoto wengi. Lakini anafanya hilo ni jambo lenye kumghafilisha kiasi cha kwamba hali yake inakuwa:

أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ حَتَّىٰ زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ

“Kumekughafilisheni kushindana kutafuta kwa wingi mpaka [tahamaki] mkayazuru makaburi.” 102:01-02

Mtu kama huyu furaha haikuhakikika kwake.

Wengi wetu pia tumedhani kuwa furaha inapatikana kwa kukusanya michezo mbalimbali majumbani. Matokeo yake tunaziletea famili zetu michezo mbalimbali kwa lengo la kudhania kwetu tutawafurahisha. Hata hivyo furaha haihakikiwi.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy§
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab sa´aadat-il-Usrah, uk. 13-15
  • Imechapishwa: 08/10/2016