02. Kujionyesha na kutaka kusikika


Kujionyesha ni shirki iliojificha kwa sababu inahusiana na makusudio na nia ambayo hakuna awezaye kuyajua isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kujionyesha kumefungamana na kuonekana; mwenye kujionyesha anakipamba kitendo chake ili aweze kuonekana, kusifiwa, kutapwa na mengineyo. Haya yanaitwa kujionyesha kwa sababu anakusudia watu waweze kumuona.

Tofauti ilioko kati ya kujionyesha na kutaka kusikika (السمعة) ni kwamba kujionyesha kunahusiana na matendo yanayoweza kuonekana ambayo uinje wake yanafanywa kwa ajili ya Allaah na undani wake yamefanywa kwa ajili ya malengo mengine. Mfano wa matendo hayo ni kama swalah na swadaqah.

Ama kutaka kusikika kunahusiana na yale maneno yanayoweza kusikiwa ambayo uinje wake yanafanywa kwa ajili ya Allaah na undani wake yamefanywa kwa ajili ya malengo mengine. Mfano wa matendo hayo ni kisomo, adhkaar na mawaidha. Malengo ya yule mzungumzaji ni watu wayasikia maneno yake na baadaye wamsifie na kumtapa katika maneno yake, majadiliano, khutbah, ana sauti nzuri wakati wa kusoma Qur-aan na kadhalika. Ikiwa anatoa mihadhara, nad-wah na darsa kwa lengo watu wamsifu. Hii ndio huitwa kutaka kusikika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 439-440
  • Imechapishwa: 16/08/2019