02. Kuingia kwa Ramadhaan kunathibiti kupitia mtu mmoja?

Swali 02: Kuingia kwa Ramadhaan kunathibiti kupitia mtu mmoja?

Jibu: Ndio. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikubali kuingia kwa Ramadhaan kupitia ushahidi wa bedui mmoja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia:

“Unashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba mimi ni Mtume wa Allaah?” Mtu yule akasema: “Ndio.” Baada ya hapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaamrisha watu wafunge.”[1]

[1] Abu Daawuud (2340), at-Tirmidhiy (691), an-Nasaa’iy (2112), Ibn Maajah (1652) na ad-Daarimiy (1692). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (907).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 11/06/2017