Swawm inaanza ima kwa kuona mwezi mwandamo wa Ramadhaan au kwa kukamilisha Sha´baan siku thelathini. Ikiwa mwezi mwandamo hauwezi kuonekana kwa sababu ya mawingu au ukungu, basi swawm haianzi siku ya kufuata. ´Ammaar bin Yaasir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Yule mwenye kufunga siku ambayo inatiliwa shaka basi amemwasi Abul-Qaasim (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Siku ambayo inatiliwa shaka ni tarehe 30 Sha´baan. Si halali kufunga tarehe 30 Sha´baan ikiwa mwezi mwandamo hauwezi kuonekana kwa sababu ya mawingu au ukungu. Ama mwezi mwandamo usipoonekana pamoja na kutokuweko mawingu na ukungu, basi siku inayofuata ni siku isiyokuwa na shaka yoyote kwa sababu kwa sababu inatambulika wazi kuwa ni katika Sha´baan. Kwa vile mwezi mwandamo wa Ramadhaan haukuonekana pamoja na kutokuweko kizuizi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mukhtaswar ´alaa Buluugh-il-Maraam (2/406)
  • Imechapishwa: 21/04/2020