02. Hadiyth “Yule atakayelazimiana na Rak´ah kumi na mbili mchana na usiku… “

580- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayelazimiana na Rak´ah kumi na mbili mchana na usiku, basi ataingia Peponi: Rak´ah nne kabla ya Dhuhr, mbili baada yake, mbili baada ya Maghrib, mbili baada ya ´Ishaa na mbili kabla ya swalah ya Fajr.”[1]

Ameipokea an-Nasaa’iy na tamko ni lake, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah kupitia kwa al-Mughiyrah bin Ziyaad, kutoka kwa ´Atwaa’, kutoka kwa ´Aaishah. an-Nasaa’iy amesema:

“Hili ni kosa. Huenda amekusudia ´Anbasah bin Abiy Sufyaan lakini akaandika makosa.”[2]

Kisha akaipokea an-Nasaa’iy kupitia kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa ´Atwaa’, kutoka kwa ´Anbasah bin Abiy Sufyaan, kutoka kwa Umm Habiybah na akasema:

“´Atwaa’ bin Abiy Rabaah hakuisikia kutoka kwa ´Anbasah.”

[1] Swahiyh kupitia zengine.

[2] Namna hii ndivo ilivo katika ile ya asili. Kuna kitu kisichokuwa wazi kinachodhihiri katika “at-Takhiysw al-Habiyr” kwamba an-Nasaa´iy alisema:

”Hili ni kosa. Huenda ´Atwaa´ alimaanisha ”Kutoka kwa ´Anbasah” ambapo anaandika makosa kwamba ni ´Aaishah”.”

Bi maana Hadiyth imepokelewa na Umm Habiybah na sio ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/377-378)
  • Imechapishwa: 08/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy