146- Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Tahadharini na sehemu tatu zilizolaaniwa. kufanya haja kubwa karibu na maeneo ya maji, kwenye njia au katika vivuli.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud na Ibn Maajah kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Humayriy, kutoka kwa Mu´aadh. Abu Daawuud ambaye amesema:

“Kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi.”

Bi maana Abu Sa´iyd hakuwahi kukutana na Mu´aadh[2].

al-Khattwaabiy amesema:

“Makusudio ya vivuli hapa ni vile vivuli ambavo vimefanywa na watu kulala usingizi wa mchana na kupiga kambi. Haina maana kwamba ni haramu kukidhi haja chini ya vivuli vyote, kwa sababu Mtume Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikidhi haja yake chini ya kikundi cha mitende –  haiwezekani kukakosa kivuli.”[3]

[1] Nzuri kupitia zengine.

[2] Lakini inashuhudiwa na Hadiyth ya Ibn ´Abbaas mfano wake inayokuja baada yake. Kila moja inaipa nguvu nyingine. Pia ina cheni za wapokezi nyenginezo zinazoitia nguvu ambazo nimezitaja katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl”(01/100-102).

[3] Ma´aalim-us-Sunan (1/39).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/171-172)
  • Imechapishwa: 10/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy