02. Hadiyth “Sijawahi kumuona Mtume wa Allaah akiliendea mbio jambo… “

582- Kutoka kwake amesema:

“Hakuna kitu katika swalah za sunnah ambacho Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikitilia mkazo zaidi kuliko Rak´ah mbili za kabla ya Fajr.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy na Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake. Katika upokezi wa Ibn Khuzaymah imekuja:

“Sijawahi kumuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiliendea mbio jambo la kheri wala mateka kama Rak´ah mbili za kabla ya Fajr.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/379)
  • Imechapishwa: 08/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy