02. Hadiyth “Peponi upo mlango unaoitwa ar-Rayyaan… “


979- Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Peponi upo mlango unaoitwa ar-Rayyaan. Wataingia kupitia mlango huo wafungaji siku ya Qiyaamah na si wengine. Watapoingia utafungwa na hakuna mwengine atakayeingia.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, an-Nasaa´iy na at-Tirmidhiy ambaye ana ziada:

“Atakayeingia kamwe hatopata kiu.”

Imepokelewa vilevile na Ibn Khuzaymah kwa tamko lisemalo:

“Atakapoingia yule wa mwisho wao utafungwa. Atakayeingia atakunywa na atakayekunywa kamwe hatopatwa na kiu.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (01/577)
  • Imechapishwa: 27/05/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy