38- Abu Shurayh al-Khuzaa´iy amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijitokeza kwetu na akasema: “[Pateni bishara!] Nyinyi hamshuhudii ya kwamba hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah na kwamba mimi ni Mtume wa Allaah?” Tukasema: “Ndio.” Akasema: “Hakika hii Qur-aan [ni kamba]; ncha yake moja iko mikononi mwa Allaah na ncha yake nyingine iko mikononi mwenu. Shikamaneni nayo; hakika hamtopotea na wala hamtoangamia baada yake kamwe.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” kwa cheni ya wapokezi nzuri[2].

[1] Swahiyh.

[2] Imepokelewa vilevile na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na Ibn Naswr katika ”Qiyaam-ul-Layl” kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Ziada mbili ziko kwa wote wawili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/453)
  • Imechapishwa: 26/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy