02. Hadiyth “Kitu bora anachoweza mtu kuacha baada ya kuondoka kwake ni mambo matatu… “

113- Abu Qataadah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kitu bora anachoweza mtu kuacha baada ya kuondoka kwake ni mambo matatu; mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa, swadaqah yenye kuendelea ambayo ujira wake unamfikia na elimu inayotendewa kazi baada kuondoka kwake.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

Pia imekwishatangulia Hadiyth ya Abu Hurayrah:

“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake yote yanakatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika kwayo au mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa.”

Ameipokea Muslim.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/156)
  • Imechapishwa: 03/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy