02. Hadiyth “Ikiwa siku ya ijumaa ambapo mtu akaoga… “


705- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ikiwa siku ya ijumaa ambapo mtu akaoga na akaosha kichwa chake, akajipata katika manukato yake mazuri na akavaa katika mavazi yake mazuri, kisha akatoka kwenda katika swalah, asijipenyeze kati ya watu wawili halafu akamsikiliza imamu, anasamehewa kutokea ijumaa hiyo mpaka ijumaa nyingine na ukiongezea siku tatu.”

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/442)
  • Imechapishwa: 17/01/2018