02. Hadiyth “Hakuna yeyote mwenye kutoka nyumbani kwake kwa ajili ya kutafuta elimu… “

85- Zirr bin Hubaysh amesema:

“Nilimwendea Swafwaan bin ´Assaal al-Muraadiy (Radhiya Allaahu ´anh) ambapo akasema: “Kipi kimekuleta?” Nikasema: “Kutafuta elimu.” Ndipo akasema: “Hakika mimi nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Hakuna yeyote mwenye kutoka nyumbani kwake kwa ajili ya kutafuta elimu isipokuwa Malaika huziweka mbawa zao juu ya mwanafunzi wakiwa ni wenye kuridhia kile anachokifanya.”[1]

Ameipokea at-Tirmidhiy ambaye ameisahihisha, Ibn Maajah na tamko ni lake, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na al-Haakim aliyesema:

“Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/145)
  • Imechapishwa: 29/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy