02. Hadiyth “Hakika si katika wema mkafunga katika safari… “

1054- Vilevile yeye huyohuyo amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa katika safari ambapo akamuona bwana mmoja watu wamekusanyika juu yake na wamemfanyia kivuli ambapo akasema: “Ana nini huyu?” Wakasema: “Ni mtu amefunga.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Si wema kufunga safarini.”[1]

Katika upokezi mwingine kumezidishwa:

“Lazimianeni na ruhusa ya Allaah ambayo amekupeni.”[2]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Si katika wema kufunga safarini.”

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud na an-Nasaa’iy.

Katika upokezi wa an-Nasaa´iy imekuja:

“Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpitia bwana mmoja aliyekuwa chini ya kivuli cha mti na akinyunyiziwa maji. Akasema: “Ana nini rafiki yenu?” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Amefunga.” Ndipo akasema: “Hakika si katika wema mkafunga katika safari. Lazimianeni na ruhusa ya Allaah aliyokupeni na muikubali.”[3]

[1] Swahiyh.

[2] Ziada hiyo ipo kwa an-Nasaa´iy peke yake. Nimeyataja hayo katika “Irwaa’-ul-Ghaliyl” (4/54-57).

[3] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/614-615)
  • Imechapishwa: 21/04/2020