02. Hadiyth “Ataletwa mtu siku ya Qiyaamah… “

124- Usaamah bin Zayd (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Ataletwa mtu siku ya Qiyaamah na kuvugumizwa Motoni ambapo matumbo yake yatatoka nje. Atazunguka nayo kama punda anavozunguka kwenye kinu chake. Watu wa Motoni watakusanyika kwake na kusema: “Ee fulani! Una nini? Wewe si ulikuwa ukiamrisha mema na ukikataza maovu?” Aseme: “Nilikuwa nikikuamrisheni mema lakini mimi mwenyewe siyafanyi na nikikukatazeni maovu lakini lakini mimi mwenyewe nayafanya.”[1]

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/161)
  • Imechapishwa: 05/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy