02. Du´aa ya kuamka kutoka usingizini

  Download

1-

الْحَمْدُ للَّهِ الَّذِي أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا، وَإِلَيْهِ النُّشُورُ

“Hidmi zote anastahiki Allaah ambaye ametupa uhai baada ya kutufisha na Kwake ndiko tutafufuliwa.”[1]

2-

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَريكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَىكُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ للَّهِ، وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكبَرُ، وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ الْعَلِيِّ الْعَظِيمِ، رَبِّ اغْفرْ لِي

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa ni Mmoja pekee asiyekuwa na mshirika, ni Wake ufalme, ni Zake himdi Naye juu ya kila jambo ni muweza. Kutakasika kutokamana na mapungufu ni kwa Allaah, himdi zote ni Zake, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, Allaah ni mkubwa na hapana hila wala nguvu isipokuwa kwa uwezo wa Allaah, Aliyejuu kabisa, Aliyemtukufu, ee Mola nisamehe.”[2]

3-

الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي عَافَانِي فِي جَسَدِي، وَرَدَّ عَلَيَّ رُوحِي، وَأَذِنَ لي بِذِكْرِهِ

“Himdi zote anastahiki Allaah ambaye amenipa afya katika mwili wangu, akanirudishia roho yangu na akaniruhusu kumtaja.”[3]

4-

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ  الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ  رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلْإِيمَانِ أَنْ آمِنُوا بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا ۚ رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الْأَبْرَارِ رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَىٰ رُسُلِكَ وَلَا تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّكَ لَا تُخْلِفُ الْمِيعَادَ

“Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na mabadiliko ya kufuatana usiku na mchana, bila shaka ni alama kwa wale wenye akili; ambao wanamdhukuru Allaah kwa kusimama  na kwa kukaa na kwa kulala ubavuni mwao na wanazingatia katika kuumbwa mbingu na ardhi [na huku wakisema]: “Ee Mola wetu! Hukuumba haya bure – kutakasika ni Kwako tukinge na adhabu ya Moto. Ee wetu! Hakika muingizaye Motoni hakika umemtweza na madhalimu hawana yeyote mwenye kuwanusuru. Ee Mola wetu! Hakika sisi tumemsikia mwenye kunadi akiita katika imani kwamba ‘mwaminini Mola wenu’ ambapo tukaamini.  Ee Mola wetu! Tusamehe madhambi yetu na tufutie makosa yetu na tufishe pamoja na waja wema. Ee Mola wetu Tupe uliyotuahidi kupitia Mitume Yako wala usitutweze siku ya Qiyaamah – hakika Wewe huendi kinyume na miadi… “[4]

[1] al-Bukhaariy (6314) na Muslim (2711).

[2] Atakayesema hivo atasamehewa na du´aa yake itapokelewa. Akiamka basi atawadhe kisha aombe kabla ya kuswali. al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (03/39) kwa nambari. 1154 na wengineo. Tamko ni la Ibn Maajah. Tazama “Swahiyh Ibn Maajah” (02/225).

[3] at-Tirmidhiy (3401). Tazama “Swahiyh at-Tirmidhiy” (03/114).

[4] 03:190-200

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 09/06/2018