02. Dalili juu ya mguu wa Allaah 2

2- Muhammad bin Makhlad bin Hafsw ametuhadithia: Muhammad bin Ishaaq as-Swaghaaniy ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdillaah bin Ibraahiym ametuhadithia: Abu Qabiyswah Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan bin ´Ammaar bin al-Qa´qaa´ na al-Husayn bin Shaakir ametuhadithia: ´Abdullaah bin ´Umar ametuhadithia: Haramiy bin ´Umaarah ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kutatupwa Motoni na useme:

هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Hakuna zaidi?”[1]

mpaka Mola wa walimwengu aweke mguu Wake – au unyayo Wake – ndani yake ambapo utasema: “Tosha, tosha.”

[1] 50:30

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 36-38
  • Imechapishwa: 18/10/2017