Kwa ajili hii Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema mwanzoni mwa “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”:

“Shukurani zote njema anastahiki Allaah ambaye amefanya katika kila kipindi cha kukatika kwa utume kuwepo kwa wanachuoni. Wanakilinda Kitabu cha Allaah kutokamana na makengeusho ya wapetukaji, maneno ya watu wa batili na tafsiri za kimakoza wa wajinga. Wanawalingania waliopotea katika uongofu na wanavumilia juu ya maudhi yao. Ni wapotevu wangapi wamewaongoza! Ni wafu wangapi waliouawa na Ibliys wamewahuisha! Ni athari nzuri ilioje walionayo kwa watu na ni athari mbaya ilioje watu walionayo kwao!”

Miongoni mwa watu hawa ambao wasifu huu mkubwa wa Imaam Ahmad unaweza kutumiwa kwao ni Shaykh-ul-Islaam, Imaam na Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah). Alishika msimamo barabara inapokuja katika kubadilisha mageuzo ya mambo mepya katika jamii yake. ´Aqiydah ilikuwa imekumbwa na upindaji. Hukumu ilikuwa imegawanyika kati ya watu. Ada za kipindi cha kikafiri zilikuwa zimeenea katika miji na katika vijiji. Mambo ya shirki katika ´ibaadah. Watu walikuwa ni wenye kwenda kinyume na Shari´ah. Mambo ya urozi na uchawi vilikuwa ni vyenye kuenea. Jambo la kuamrisha mema na kukataza maovu lilikuwa ni lenye kuachwa, seuze wanachuoni wengi walikuwa kati yao. Walikuwepo wanachuoni wengi waliobobea katika mambo yanayohusiana na matawi. Kinachozingatiwa sio uwepo wa wanachuoni midhali hawana athari yoyote katika kutengeneza. Wana wa israaiyl waliangamizwa pamoja na kwamba kulikuwepo wanachuoni kati yao. Wakati walikuwa si wenye kutimiza wajibu wao katika kuwatakia watu mema na kutengeneza, ndipo shaytwaan akawatawala. Amesema (Ta´ala):

وَتَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يُسَارِعُونَ فِي الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ لَوْلَا يَنْهَاهُمُ الرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ عَن قَوْلِهِمُ الْإِثْمَ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَصْنَعُونَ

”Utawaona wengi miongoni mwao wanakimbilia katika dhambi na uadui na kula kwao haramu; bila shaka mabaya mno waliyokuwa wanatenda! Kwa nini hawawakatazi viongozi na marabi wao kuhusu kauli zao za dhambi na ulaji wao wa haramu? Hapana shaka ni mabaya mno waliyokuwa wanatimiliza!”[1]

Wakati imamu huyu aliposimama kidete dhidi ya jamii yake iliokuwa imepinda, kusimama kwa ukweli na kwa kuwatakia watu mema, ndipo akausafisha na yale yote yenye kuuangamiza. Haya pamoja na kwamba alikuwa ni mtu mmoja tu. Lakini mshairi amesema:

Watu elfumoja ni kama mtu mmoja

na mmoja ni kama elfumoja akiwa sirias

Namna hii ndivo mwenendo wa Allaah, haubadiliki. Ummah hauwezi kunyanyuka wala kuamka isipokuwa kwa tawfiyq ya Allaah kisha kwa juhudi za wanachuoni wake wenye Ikhlaasw na walinganizi wenye kuwatakia watu mema. Allaah amrehemu Imaam Maalik ambaye amesema:

“Hautofaulu mwisho wa Ummah huu isipokuwa kwa yale yaliyofanya wa mwanzo wao kufaulu.”

Tofauti iliopo kati ya Ummah huu na nyumati zengine ni kwa kusimama na jambo la kutengeneza na kulingania kwa Allaah:

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu. Hao ndio waliofaulu.”[2]

[1] 05:62-63

[2] 03:104

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 10-11
  • Imechapishwa: 24/06/2019