02. Adabu ya pili: kujiepusha na mikhalafa


Ni wajibu kwa mwanafunzi ajitwaharishe udhahiri wake kwa kujiepusha na Bid´ah na badala yake kujipamba na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika hali zake zote. Vilevile mwanafunzi anatakiwa kuhifadhi wudhuu´, kujisafisha mwili na muonekano wake pasi na kujikalifisha. Afanye hivo kadri na uwezo wake.

Ibn Abiy Haatim amesimulia: ´Abdullaah bin Abiy ´Umar al-Bakriy ameeleza kuwa amemsikia ´Abdul-Malik al-Maymuuniy akisema:

“Sijui kama nimeshawahi kumuona mtu aliye na nguo safi zaidi na mwangalifu zaidi kwake mwenyewe, katika kinywaji chake, nywele za kichwani mwake, nywele za mwilini mwake na mwenye mavazi yaliyo masafi na meupe zaidi kama Ahmad bin Hanbal. Hilo ni kwa sababu Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) alikuwa akitikisika na kutulia kwa mujibu wa Sunnah. Amesema (Rahimahu Allaah):

“Sikuandika Hadiyth hata moja isipokuwa niliitendea kazi. Mpaka nilifikiwa na khabari kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliumikwa na akampa Abu Twaybah dinari moja, nami nikampa aliyenifanyia chuku pindi nilipoumikwa.”

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Sa´iyd Raslaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadab Twaalib-ul-´Ilm, uk. 29
  • Imechapishwa: 23/04/2017