Swali 1: Nini unachowanasihi ndugu waheshimiwa ambao wanashiriki katika vituo vya kiangazi ikiwa [vikao hivyo] vinagongana na darsa za wanazuoni? Je, wahudhurie katika darsa au wabaki katika vituo hivyo? Tunatarajia jibu la kina kwa sababu vijana wengi wanazungumzia juu ya suala hili.

Jibu: Malengo ya vituo ni kuwasafisha na kuwafunza wanafunzi. Ninaonelea kwamba wasimamizi wa vituo wanatakiwa kutenga wakati wawapeleke vijana katika misikiti ili waweze kusikiliza mihadhara na darsa. Kwa sababu kuhudhuria katika mihadhara ni sehemu ya vituo hivi. Badala ya muhadhiri kuwaendea wao wanatakiwa kwenda katika mihadhara misikitini. Hili ni bora. Ni bora kwao wakahudhuria msikitini, katika nyumba ya Allaah na kusikiliza elimu ni bora kuliko kubaki kwenye vituo[1].

Kwa kuhitimisha ni kwamba ni wajibu kwa wale wasimamizi wa vituo kupanga barnamiji ili mihadhara katika misikiti ipate wakati wake na isigongane na mihadhara. Hili ni kama tulivyosema ya kuwa ni moja katika malengo ya vituo vya kiangazi.

[1] Hapo zamani misikiti ilikuwa ndio chimbuko la elimu na kituo cha wanazuoni. Kutokea hapo ndio kumetoka wanazuoni ambao walikuwa vigogo katika elimu ya Hadiyth, Fiqh na misingi yake, tafsiri na misingi yake, sarufi na fani zake. Wale waliokuwa na elimu zote hizi mara nyingi wote walikuwa wanatoka kwenye mizunguko ya kielimu misikitini. Kila mmoja anapaswa kujua kuwa elimu inaendewa na haiwaendei watu. Hivyo basi, msibadilishe kilicho kibaya kwa kilicho bora.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 08/10/2016