01. Uwajibu wa kuyajua mambo kumi yanayochengua Uislamu

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tambua ya kwamba mambo yanayochengua Uislamu ni kumi.”

MAELEZO

Hapa kunaamrishwa elimu. Elimu ni hukumu ya akilini kwa njia ya kukata. Bi maana yakini. Kwa msemo mwingine tambua na uwe na yakini ya kwamba Uislamu unachenguka kwa kufanya moja katika mambo haya kumi yenye kuchengua Uislamu. Kuwa na elimu kinyume chake ni kuwa na dhana. Elimu kwa maana nyingine ni yakini. Kuwa na yakini na utambue kuwa mtu akifanya moja katika mambo haya kumi yenye kuchengua Uislamu anatoka katika Uislamu. Kuwa na utambuzi wa kukata kabisa pasi na shaka, ubabaikaji na dhana. Bali kinyume chake unatakiwa utambue kwa kukata kabisa ya kwamba Uislamu unachenguka kwa kufanya moja katika mambo haya kumi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tabswiyr-ul-Anaam bisharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 11
  • Imechapishwa: 09/04/2023