01. Utangulizi wa Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib ya Ibn Taymiyyah

Allaah! Mswalie kiumbe Chako bora Muhammad! Himdi zote ni za Allaah na inatosheleza. Salaam na amani kwa waja Wake ambao Amewachagua. Nashuhudia ya kwamba hapana mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah Mmoja, asiyekuwa na mshirika, na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Mtume Wake.

Anasema Allaah (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ

“Enyi mlaomini! Mcheni Allaah na semeni kauli ya kweli (ya sawasawa). Atakutengenezeeni ‘amali zenu, na Atakusameheni madhambi yenu.” (al-Ahzaab 33 : :70-71)

إلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

Kwake Pekee linapanda neno zuri na kitendo chema Hukipa hadhi.” (Faatwir 35 : :10)

فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ

“Basi nidhukuruni na Mimi Nitakukumbukeni; na nishukuruni wala msinikufuru.” (al-Baqarah 02 : 152)

اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا

“Mdhukuruni Allaah kwa dhikri ya wingi.” (al-Ahzaab 33 : :41)

وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ

“Na Wanaume wanaomdhukuru Allaah kwa wingi na Wanawake wanaomdhukuru.” (al-Ahzaab 33 : 35)

الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ

“Ambao wanamdhukuru Allaah (kwa) kusimama, na (kwa) kukaa na (kwa) kulala ubavuni mwao.” (al-´Imraan 03 : 190)

إِذَا لَقِيتُمْ فِئَةً فَاثْبُتُوا وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا

“Mtapokutana na jeshi lolote (lile la makafiri), basi simameni imara, na mdhukuruni Allaah kwa wingi.” (al-Anfaal 08 : 45)

فَإِذَا قَضَيْتُم مَّنَاسِكَكُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَذِكْرِكُمْ آبَاءَكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا

“Mtakapomaliza kutekeleza manaasik zenu (‘ibaadah za Hajj), basi mdhukuruni Allaah kama mnavyowadhukuru baba zenu au mdhukuruni zaidi.” (al-Baqarah 02 : 200)

لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ

“Yasikushughulisheni mali zenu na wala watoto wenu na Dhikr ya Allaah (kumtaja na kumkumbuka).” (al-Munaafiquun 63 : 09)

رِجَالٌ لَّا تُلْهِيهِمْ تِجَارَةٌ وَلَا بَيْعٌ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَإِقَامِ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ

“Wanaume haiwashughulishi tijara (biashara) wala uuzaji na Dhikri-LLaah (kumtaja na kumkumbuka) na (hayawashughulishi pia na) kusimamisha Swalaah, na (wala) kutoa Zakaah.” (an-Nuur 24 : 37)

وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ

“Na mdhukuru Mola wako katika nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu na si kwa jahara (kunyanyua sauti) katika kauli asubuhi na jioni; na wala usiwe miongoni mwa walioghafilika.” (al-A´raaf 07 : 205)

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 19/03/2017