01. Utangulizi wa ”Aadaab-uz-Zafaaf”

Himdi zote anastahiki Allaah aliyesema katika Kitabu Chake:

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً

“Miongoni mwa alama Zake ni kwamba amekuumbieni katika jinsi yenu wake ili mpate utulivu kwao na amekujaalieni kati yenu mapenzi na huruma.”[1]

Swalah na salaam zimwendee Mtume Wake Muhammad ambaye kumepokelewa kutoka kwake katika Hadiyth:

”Oeni wanawake wenye kuzaa sana na wenye mahaba, kwani hakika mimi nitajifakhari kwa ajili yenu siku ya Qiyaamah.”[2]

Amma ba´d:

Hakika kwa yule anayetaka kuoa na akataka kumwingilia mke wake, basi atambue kuwa kuna adabu katika Uislamu. Watu wengi wameghafilika nayo au hawayajui kabisa kukiwemo wale wanaojitahidi kufanya ´ibaadah. Kwa ajili hiyo ndio maana nikapendelea kutunga kijitabu hiki chenye faida kwa mnasaba wa ndoa ya mtu ambaye ni kipenzi changu kwa lengo la kutaka kumsaidia yeye na ndugu waumini wengine ili waweze kutekeleza yale aliyoyaweka katika Shari´ah bwana wa Mitume kutoka kwa Mola wa walimwengu. Vilevile nimezindua baadhi ya mambo ambayo ni muhimu kwa kila mwenye kuoa. Kwani mambo hayo wamepewa mtihani kwayo wake wengi.

Ninamuomba Allaah (Ta´ala) anufaishe kwacho na akijaalie niwe nimekifanya kwa ajili Yake pekee – hakika Yeye ndiye Mwema na Mwenye huruma.

[1] 30:21

[2] Ahmad na at-Twabaraaniy kwa mlolongo wa wapokezi mzuri Swahiyh. Vilevile kaipokea Ibn Hibbaan kutoka kwa Anas na ina shawahidi zengine ambazo tutazitaja katika masuala ya 19.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 89
  • Imechapishwa: 22/02/2018